Breaking News
Loading...

PHOTO OF THE DAY

STUDENTS CORNER

START UP LAB

Recent Post

Showing posts with label Biashara. Show all posts
Showing posts with label Biashara. Show all posts
Wednesday, June 4, 2014
Best Ideas za kujitengenezea Mtaji wa kuanzisha Biashara ndogo Jijini Dar es Salaam.

Best Ideas za kujitengenezea Mtaji wa kuanzisha Biashara ndogo Jijini Dar es Salaam.


Best Ideas za kujitengenezea Mtaji wa kuanzisha Biashara ndogo Jijini Dar es Salaam. 

Unapofungua biashara, mtaji utakulazimu ni kwa jinsi gani unatakiwa kulipia eneo la kazi ambapo kwa wakazi wa Dar es Salaam yaweza ni kuwa na "Flame" ingawa kwa biashara ndogo nyumbani au sehemu utayoweza kuipata kwa bei sawa na bure ni eneo zuri kwa kuanzia. Piautahitaji matangazo na kuajili watu pamoja na kununua bidhaa na vifaa vya biashara yako. Wamiliki wa biashara ndogo wanataka kukuza mtaji wao kwa kuja na mawazo mbalimbali kupata mtaji wa kutosha kwa biashara yao:-

Anzisha Tukio (Event)


Unaweza kupata mtaji wa biashara yako ndogo kwa kutafuta wazo ambalo unaweza kuwa na tukio ambalo litawaleta watu wenye uhitaji unaofanana au watu wanaotoka katika jamii zitazoweza kufurahi kujumuika pamoja iwe kwa mashindano, mziki, au chakula cha jioni. Katika mji wa Dar es Salaam kuna vyama vingi mfano. vyama vya wajasiliamali wanawake, vyama vya wafanyabiashara, vyama vya waendesha magari ya aina fulani au Vyama vya wafanyakazi wa aina fulani, jumuiya mbalimbali za mitaa au magroup ya Mitandao ya Kijamii kama Facebook na Apps kama Wasap. Watoze wanaotaka kushiriki kama watu binafsi na vikundi katika tukio lako. Unaweza kutangaza Tukio lako kwa gharama ndogo kwa kutumia mitandao ya kijamii au huduma ya bure ya kutuma sms kwa watu wengi katika tovuti hii PIPIT. Pia tangaza tukio lako kwa kuweka makala katika tovuti kama ZOOMTANZANIA uweze kujitangaza katika mitandao. Ni vizuri kuchukua sehemu ndogo ya faida utayopata na kuitoa kama msaada kwa watu wasio na uwezo kwani watu wanapenda kuona wanachangia kitu ambacho ni muhimu kwa jamii unayotaka kuihudumia kibiashara. 

Read an English Version of this Article: Best Fundraising Ideas to Open a Business in Dar es Salaam.

Jichange


Kwa wafanya kazi ni vyema kujipanga kuanza kuhifadhi sehemu ya mshahara unaopata kwa ajili ya kuchangia mtaji wa biashara unayotaka kuanzisha na ufanye uamuzi wa kufikia lengo laki kiukweli.

Fanya Mauzo.


Ni kwa mara nyingi unaweza kujikuta umenunua kitu ambacho tayari unacho kama TV, Gari, Simu, nk. Hii ni nafasi ya wewe pia kuweza kuongeza kipato kwa kuuza kile ambacho huna matumizi nacho kama kitanda kilichozidi au Jiko la umeme usilotumia. Tumia mitandao ya kijamii na watu wanaokufahamu kutangaza kuwa unauza kifaa hiki. Hii itakuongezea mtaji wako na kupata ujuzi wa kimasoko kabla ya kuanza biashara yako.


Uza Uwezo/Ujuzi wako.


Maisha yanatupa ujuzi mbalimbali kama mapishi, ushonaji, kufanya mauzo, au hata kujua kufundisha watoto kujua kusoma na kuandika lakini kila mtu ana kile kipaji au ujuzi ambao watu hawasiti kusema kuwa wewe ndio mkali yaani mjuzi sana wa kitu fulani.  Tumia fursa hii kama nafasi ya wewe kuwakusanya watu 5 au 10 kuwafundindisha kile ambacho unakifahamu kwa watu ambao watakuwa tayari kujifunza kutoka kwako a kukulipa kwa muda utaotumia kuandaa na kuwafundisha.

Tafuta Suluhisho la Tatizo linalosumbua Mtaa wako 


Katika mitaa yetu kuna vitu mbalimbali ambavyo ni kero kwa nyumba 5 hadi kumi na kwa maeneo ambayo hakuna watu wengi kuna fursa maana kila mtu anakuwa yuko busy kufanya kazi zake za kila siku. Hii ni fursa kwa baadhi ya mitaa ambayo watakuwa ni waelewa unaweza tumia muda wako kutafuta fundi aje kujenga lile daraja dogo lililovunjika au mkandasi kuzibua mtaro nk. Halafu wewe ukajipatika kiasi cha asilimia 10% ya kipato cha fundi uliyemtafuta kama shukrani yake kwako

Andika Makala fupi kujitangaza nia.


Kwa kuandika makala fupi inayomuelezea mtu mwenye uwezo wa kuwekeza kwako (donor) kufafanua ni aina gani ya biashara unajaribu kuanzisha na ina ya bidhaa na huduma utazokuwa unatoa na elezea jinsi biashara yako itavyowasaidia wateja unaowatazamia. Kupata mtaji wa biashara yako ni kitu kinachowezekana. Tuma makala hii kwa marafiki, familia, vyuoni na kwa wafanyabishara wadogo wenzako. Elezea vizuri faida za kukuunga mkono, faida ambazo zaweza kuwa kuwatangaza kwa wateja wako pale wanapohitaji huduma zinazendana na huduma wanazotoa wao, kupata kuwatanga katika Blog au tovuti yako au kupata fungu katika umiliki wa bishara yako (shares).  Hakikisha umekeka mawasiliano yako kama namba ya simu na barua pepe ili waweze kukutafuta endapo watakuwa na maswali ya kukuuliza kuhusu biashara yako au kutoa msaada wowote. Pia andika jinsi ya watu watavyoweza kukuchangia mfano akaunti ya benki, au huduma za simu kama MPESA etc.

     JIPATIE MAKALA KAMA HIZI KATIKA BARUA PEPE KILA WIKI

Enter your email address:


Delivered by BusinessTOK
Best Fundraising Ideas to Open a Business in Dar es Salaam.

Best Fundraising Ideas to Open a Business in Dar es Salaam.

Best Fundraising Ideas to Open a Business in Dar es Salaam.



When you’re opening a new business, funding (capital) dictates how much money you have to pay for a location which in Dar es Salaam would be renting a space commonly known as "Flame", initiate marketing and promotional activities, hire staff and purchase supplies and equipment. Small-business owners who want to maximize their start-up funding come up with a variety of fundraising ideas to get their ventures started. 




Host an Event


You can earn money for your start-up by hosting an event, such as a brunch, dinner or cocktail party. Invite friends, family members and business colleagues to attend the event. Charge individuals and groups to attend the dinner and allow businesses to act as sponsors. You can promote your event with the Social Media and a free Tanzanian bulk sms website at PIPIT  and set up a post on  website that provides the event details and sponsorship opportunities and explains that the purpose of the event is to raise money to open your business such as ZOOMTANZANIA  Rather than keeping all of the profits from the event, you can also donate a portion of the event sales to a charity or cause that’s important to your attendees or the target market your business intends to serve. 

Save Money

For employed individuals at the moment or those with income activities of any kind, it is important to save a percent in what you get and truly commit yourself in achieving a certain target.  

Trade your most strengths

You as an individual must have a strength in something in the course if life. Be it that best cooking that your family and friends always enjoy when they come over or teaching kids how to read and write like how you did with your youngsters or children. These are often skills that we overlook and tend to be blind but i tell you that you can organize a Lesson for a group of 5 or 10 people who would like to learn that skill from you and charge them a reasonable amount for your time. This could pay off right in Dar es Salaam.

Read a Swahili Version of this Article: Best Ideas za kujitengenezea Mtaji wa kuanzisha Biashara ndogo Jijini Dar es Salaam.

Help your Community Solve problems

Do you notice the problems that your neighborhood has and cant be solve just because everybody is busy with work and don't have time? Well if you live in a fairly populated location in Dar es Salaam that is a chance for you to organize for solving the problem. Be it construction of the broken bridge shared by few households or garbage collection. You can take a chance by finding a mechanic responsible and guess what? With you mobilizing your neighbors (which is the hard part, but you'll be fine) you can get a 10%+  commission for your mechanic for such reference. 

Sale what you don't need. 

Most of the Time we find ourselves buying and owning stuff we no longer in use of. Take a chance and launch a campaign to sell the stuffs or stuff you no longer need. For your marketing lessons towards your business launch a social media campaign and bulk sms to your network promoting your product. If you have a good profit product this could be your kick-off for business in Dar es Salaam.

Also Read:  Makosa 7 yanayopelekea biashara nyingi kutofanikiwa. 


Send Sales Letters


By writing a letter that gives potential donors an explanation of the type of business you’re trying to open and the types of products and services you plan to offer and expresses how the business will help your potential clients, you can raise funds for your new business. Send your letter to friends, family, colleagues and fellow small-business owners. Highlight the benefits of participating, which may include media mentions, recognition on your website or blog or a financial stake in your business. Provide potential donors with your phone number and email address so they can contact you if they have additional questions about your business or donating, or helping you in different ways. You should also provide potential donors with various ways to donate, which may be through check, bank account, and services that mobile can offer such as Mpesa and the related.
Beware of Masterminds and people who might want to take advantage of you in Dar es Salaam hence hold your meetings at Public places and always give yourself a room to think through your decisions when meeting a  person willing to assist you. 

         Get BusinessTOK Updates right in your Email

Enter your email address:


Delivered by BusinessTOK
Saturday, May 31, 2014
no image

PHOTO OF THE DAY


Tuesday, May 27, 2014
no image

Tanzania kujipatia USD 436 Milioni kila Mwaka kupitia Mradi wa Magadi.


Tanzania to earn $436 million from soda ash

DAR ES SALAAM, Tanzania – National Development Corporation (NDC), last week announced the  government could earn Tsh720billion (about $435.9 million) annually as revenue from the Soda Ash mining project.

By Emmanuel Kisima, May 25 @BusinessWeek
NDC acting Director Heavy Industry, Ramson  Mwilangali was speaking last week. “Our findings indicate that the project could potentially generate almost Tsh480billion ($290.6 million) in revenue, from Engaruka Basin alone. And it will also generate Tsh240billion-(145.3 million) after selling 0.5 million tones of soda ash from Lake Natron,” he said.
NDC acting Managing Director Mlingi Mkucha said, the project is in the final stages of being implemented once the Environmental Impact Assessment (EIA) study is verified and approvals given. 
“We cannot start implementing this project until we are certified that environmental impact assessment has been conducted. The intention is to ensure that, decision makers consider the environmental impacts when deciding whether or not to proceed with the project,” he said.
 Detailing more benefits of the project, Mwilangali said once the project starts, the government will be able to save its foreign currency by halting purchases from Kenya.
The expert said it has been costing the government $300 per one tonne of soda ash. “So, if this project takes off, that money will be retained for other uses,” he said.
Prof. Jonathan Kabigumila, who was in charge of scientific studies on Lake Natron, said currently the human population around  in the vicinity does not pose a threat to lake resources. 
But warned that with the expected growth of tourist industry and other economic activities following construction of proposed tarmac road through area, bigger influx of immigrants may occur, which will result in putting more pressure on fragile ecosystem. 
Soda ash found in Lake Natron in being harvested by local communities for various uses, but not for industrial use. The initial plans for soda ash mining were to pump back about 9,424 cubic metres of water. The reduction of such amount of water is said by experts that would not have significant effect on the lake water balance. However Prof Kabigumila said the amount pumped back will account for only 0.2% of lake volume depending on the technology being used.
source: LINK HERE
Tuesday, May 20, 2014
5 quotes of the day: BRANDING

5 quotes of the day: BRANDING











Tuesday, May 13, 2014
Makosa 7 yanayopelekea biashara nyingi kutofanikiwa.

Makosa 7 yanayopelekea biashara nyingi kutofanikiwa.

Kuanzisha biashara kwa watu wengi ni changamoto ambayo hawawezi kuikabili. Kuanzisha biashara yako binafsi yaweza kukuletea faida kwa njia nyingi ikiwemo kujitambua zaidi, kupata uhuru za kifedha (financial independence), fursa ya kuweka alama (mark) katika maisha yako na pia kuwa katika nafasi ya kutoa mchango chanya katika jamii yako au sehemu ya kibiashara.

Katika kufikia hayo watu wengi hufikia kuanzisha biashara zenye mafanikio na nyingine bila mafanikio. Makala hii inakuletea sababu tano za kwanini biashara nyingi ndogo hushindwa kufanikiwa:-

1. Kutofanya Utafiti wa kimasoko

Biashara nyingi hushindwa kufanikiwa kwa sababu ya kutofanya utafiti wa kutosha wa kimasoko (market) ambayo hupelekea mfanyabiashara kuingia katika biashara yenye watu wafanyabiashara wengi tayari au biashara ambayo wateja hawapo na uelewa mzuri juu yake, eneo (location) ambayo sio sahihi. Hasara ambazo mtu anaweza pata kwa sababu ya kujiingiza katika biashara bila kufanya utafiti.
Bila utafiti mfanyabiashara anaweza kuanza kuuza vifaa vya kisasa kama simu, Tablets na computer katika kijiji kisicho na umeme au kuuza bidhaa maarufu kama adidas, Gucci na Macintosh kwa wateja wasio na TV. Biashara yako inatakiwa iangalie matatizo au watu wanachohitaji kutokana na mazingira yao.

2.  Nafasi ya kisheria ya biashara husika.

Kosa lingine ni Mara nyingi wajasiriamali huingia katika biashara bila kufuatilia sheria inasemaje juu ya biashara hiyo kwenye eneo analotaka kufanyia biashara, wanashindwa kufuatilia taratibu za utunzaji wa mazingira na upatikanaji wa ruhusa mfano biashara za kusafirisha mizigo, mkaa, na biashara ndogondogo katika maeneo ya mijini (mfano, Dar es Salaam).

Pia hapa tunazungumzia ulipaji wakodi au usajili wabiashara hiyo kupitia usajili wa biashara ambayo sio sahihi kulinganisha na kipato cha biashara hiyo. Mfanyabishara anatakiwa kufuatilia msamaha wa kodi na ajue ni usajili wa aina ipi waweza kumsaidia kwa kumtoza kodi halali na yenye unafuu kutokana na umri wa biashara yake na faida anayopata.
  
3.  Eneo (location) na kuwafikia wateja

Uamuzi wa uuze wapi bidhaa zako ni rahisi, inatakiwa iwe eneo amablo watu wataweza kukufikia kirahisi. Inatakiwa iwe located sehemu ambayo watu wana uhitaji wa hiyo bidhaa. Iwe mahala ambapo wewe kama mfanyabiashara waweza pata bidhaa unazouza au rasilimali za biashara yako kirahisi.

4.   Kushindwa kuanza kama biashara ndogo.

Ubora wa bidhaa ni kuwa sahihi kwa lengo husika. Sio lazima kuanza biashara kwa kununua flame au kununua duka ambalo ni Fixed Assets, watu wengi hujaribu kuanza kwa kuwa mobile mara nyingine si kwa kupenda lakini hii husaidia kutengeneza custumer base kabla hawajakuza biashara yake.
Biashara ndogo ndogo zinazoanza bila Fixed Assets zinanafasi kubwa ya kukua na kulitambua soko kuliko zile zinazoanza kwa fixed assets.

5. Kuwa na nidhamu ya kifedha (Financial discipline)

Kuwa mfanyabishara mkubwa unatakiwa kuwa na uelewa wa kujaza fomu na documents nyingi mbalimbali za kimahesabu lakini haimaanishi kwamba utakuwa na uelewa wa biashara yenyewe. Watu wanaweza kuanzisha biashara bila ya kuwa na uwezo wakujaza au kusoma balance sheet au business plan.

Uelewa kiasi wa vitu hivi ndio unaohitajika pale mfanyabiashara anapohitaji mkopo huhitajika kwenda kueleza ni jinsi gani ataweza kutunza kiasi cha faida atayopata kabla hajapata mkopo.

Wafanyabiashara wadogo wadogo hukosa mikopo kwa kutojua jinsi ya kufanya mahesabu madogo na kuwa na nidhamu katika uhifadhi wa pesa.

6. Kukosa Ushauri wa mtu mwenye uzoefu (Mentor support, Second Opinion)

Wafanyabishara wengi hukosa kujikosoa kwani kwa kuwa tupo katika nchi yenye watu masikini basi wafanya biashara huweka eneo lake la biashara au bidhaa zake juu ya wateja na kuwadhalau wateja. Mteja ni mfalme kwa hiyo mfanyabishara anatakiwa kujikosoa kwa kuwauliza baadhi ya wateja wake kwa njia tofauti za kukusanya maoni.

Kwa mtu kuamua kutumia pesa yake kwako yahitaji awe atambue unajali. Wafanyabishara wengi wanashindwa kujua kwamba wateja wanatambua kuwa kitendo cha wao kununua kwako wanachukua hatua ya kuwa-support na kudhani au kuwa-treat kana kwamba wateja hao hawana sehemu nyingine ya kwenda kujipatia mahitaji hayo.

7.  Teamwork and Networking

Katika ushindani ulipo sasa hivi ni vizuri mfanyabiashara kujiunga katika vikundi mbalimbali ili aweze kujitangaza pamoja na kuwajua wafanyabishara wenzake ambao wanaweza kumsaidia kwa mawazo na hata kwa wateja pale wanapoishiwa bidhaa Fulani katika maduka yao.

Haya ni makosa 7 ambayo wafanyabishara wadogo au wanaoanza huyafanya kwa kujua au bila kujua. Kwa kufuatilia BusinessTOK utapata kuwasikiliza wafanya biashara wataoweza kuongelea mada hii.


Usisite kuweka maoni yako juu ya makala hii hapa chini.
Back To Top