Breaking News
Loading...

EABMTI - School of Broadcasting Journalism

Background: 

EABMTI School of Broadcasting Journalism ni Mradi wa Mafunzo ya Uandishi wa Habari za Television na Radio. Mradi huu uko chini ya Chuo Cha Biashara na Uandishi cha East Africa Business and Media Training Institute (EABMTI) kilichopo mjini Dar es Salaam kilichoanzishwa rasmi mwaka 2009. 

Lengo/Mission

Lengo kuu la kuanzisha mradi huu ni kuchangia katika kuzalisha waandishi wa habari makini wa Television na Radio yaani Broadcasting, watakaoweza kushindana katika soko la Ajira la ndani na Nje.

Tayari kuna Vyombo kadhaa hapa nchini vinavyotafuta waandishi wa habari makini na wenye uwezo mkubwa wa kiutendaji. Chuo hiki kinamuandaa mwandishi ili kuweza kujiuza kwa waajiri na hata kuweza kujiajri mwenyewe, kwa wale watakaotaka kujitegemea.

Courses Offered and Duration 

EABMTI School of Broadcasting Journalism ni Chuo kinachotoa Mafunzo katika Ngazi zifuatazo:

Certificate in Broadcasting Journalism/ Cheti
Qualification hii hutolewa baada ya Mafunzo ya mwaka mmoja, yaliyogawanywa katika mihula 4 ya miezi mitatu mitatu. Kila muhula unajitegemea. Sifa za kuingia katika masomo haya mwanafunzi ni lazima awe amemaliza kidato cha nne na kufaulu masomo matatu katika kiwango cha daraja la nne.

Diploma in Broadcasting Journalism
Qualification hii inapatikana baada ya kuhitimu mafunzo ya miaka miwili ya Uandishi wa habari na Utangazaji wa Radio na Television. Sifa za mwanafunzi ni awe amemaliza kidato cha sita na kupasi katika kiwango cha daraja la tatu yaani C ama awe amehitimu na kufaulu masomo ya Uandishi wa habari katika ngazi ya Cheti.

Computer Laboratory 
Computer moja /Mwanafunzi Mmoja

Mfumo wa Kufundishia
Chuo chetu kinatumia mfumo wa kufundishia wa 20 by 80. Yaani asilimia 20 ya mafunzo yatakuwa ni maelekezo tu na 80 ni mafunzo kwa vitendo. Kimsingi chuo chetu kinatumia mfumo wa vitendo zaidi katika kufundishia wanafunzi, lengo ni kuzalisha watenda kazi zaidi kuliko wasomi wa vyeti na makaratasi.

Lugha ya Kufundishia
EABMTI School of Broadcasting Journalism itafundisha masomo yake kwa lugha ya kiswahili kwanza ili kukidhi mahitaji ya soko la ndani. Kutakuwa na kozi maalum za kiingereza kwa wanafunzi wanaolenga kuteka soko la nje.

The Classes 
Chuo kina maabara ya kutosha zikiwemo maabara za Computer na Studio za mafunzo kwa ajili ya Radio na Television.

Mihula ya Chuo:
Chuo kinafunguliwa Jumatatu Tarehe 2 Juni 2014 kwa madarasa ya Certificate na Diploma. Hata hivyo kutakua na kozi za maandalizi yaani foundations kwa wale wote wanaotaka kuhamia na kujiandaa kwa kozi zetu.

Contact: 
Msasani Peninsular Kimweri Road, Plot 2054/5 Drop at Fitness Center Bus Stop 
Contact: 0717 190 856 / 0756 488 8346
Back To Top