Breaking News
Loading...
Wednesday, June 4, 2014

Best Ideas za kujitengenezea Mtaji wa kuanzisha Biashara ndogo Jijini Dar es Salaam.


Best Ideas za kujitengenezea Mtaji wa kuanzisha Biashara ndogo Jijini Dar es Salaam. 

Unapofungua biashara, mtaji utakulazimu ni kwa jinsi gani unatakiwa kulipia eneo la kazi ambapo kwa wakazi wa Dar es Salaam yaweza ni kuwa na "Flame" ingawa kwa biashara ndogo nyumbani au sehemu utayoweza kuipata kwa bei sawa na bure ni eneo zuri kwa kuanzia. Piautahitaji matangazo na kuajili watu pamoja na kununua bidhaa na vifaa vya biashara yako. Wamiliki wa biashara ndogo wanataka kukuza mtaji wao kwa kuja na mawazo mbalimbali kupata mtaji wa kutosha kwa biashara yao:-

Anzisha Tukio (Event)


Unaweza kupata mtaji wa biashara yako ndogo kwa kutafuta wazo ambalo unaweza kuwa na tukio ambalo litawaleta watu wenye uhitaji unaofanana au watu wanaotoka katika jamii zitazoweza kufurahi kujumuika pamoja iwe kwa mashindano, mziki, au chakula cha jioni. Katika mji wa Dar es Salaam kuna vyama vingi mfano. vyama vya wajasiliamali wanawake, vyama vya wafanyabiashara, vyama vya waendesha magari ya aina fulani au Vyama vya wafanyakazi wa aina fulani, jumuiya mbalimbali za mitaa au magroup ya Mitandao ya Kijamii kama Facebook na Apps kama Wasap. Watoze wanaotaka kushiriki kama watu binafsi na vikundi katika tukio lako. Unaweza kutangaza Tukio lako kwa gharama ndogo kwa kutumia mitandao ya kijamii au huduma ya bure ya kutuma sms kwa watu wengi katika tovuti hii PIPIT. Pia tangaza tukio lako kwa kuweka makala katika tovuti kama ZOOMTANZANIA uweze kujitangaza katika mitandao. Ni vizuri kuchukua sehemu ndogo ya faida utayopata na kuitoa kama msaada kwa watu wasio na uwezo kwani watu wanapenda kuona wanachangia kitu ambacho ni muhimu kwa jamii unayotaka kuihudumia kibiashara. 

Read an English Version of this Article: Best Fundraising Ideas to Open a Business in Dar es Salaam.

Jichange


Kwa wafanya kazi ni vyema kujipanga kuanza kuhifadhi sehemu ya mshahara unaopata kwa ajili ya kuchangia mtaji wa biashara unayotaka kuanzisha na ufanye uamuzi wa kufikia lengo laki kiukweli.

Fanya Mauzo.


Ni kwa mara nyingi unaweza kujikuta umenunua kitu ambacho tayari unacho kama TV, Gari, Simu, nk. Hii ni nafasi ya wewe pia kuweza kuongeza kipato kwa kuuza kile ambacho huna matumizi nacho kama kitanda kilichozidi au Jiko la umeme usilotumia. Tumia mitandao ya kijamii na watu wanaokufahamu kutangaza kuwa unauza kifaa hiki. Hii itakuongezea mtaji wako na kupata ujuzi wa kimasoko kabla ya kuanza biashara yako.


Uza Uwezo/Ujuzi wako.


Maisha yanatupa ujuzi mbalimbali kama mapishi, ushonaji, kufanya mauzo, au hata kujua kufundisha watoto kujua kusoma na kuandika lakini kila mtu ana kile kipaji au ujuzi ambao watu hawasiti kusema kuwa wewe ndio mkali yaani mjuzi sana wa kitu fulani.  Tumia fursa hii kama nafasi ya wewe kuwakusanya watu 5 au 10 kuwafundindisha kile ambacho unakifahamu kwa watu ambao watakuwa tayari kujifunza kutoka kwako a kukulipa kwa muda utaotumia kuandaa na kuwafundisha.

Tafuta Suluhisho la Tatizo linalosumbua Mtaa wako 


Katika mitaa yetu kuna vitu mbalimbali ambavyo ni kero kwa nyumba 5 hadi kumi na kwa maeneo ambayo hakuna watu wengi kuna fursa maana kila mtu anakuwa yuko busy kufanya kazi zake za kila siku. Hii ni fursa kwa baadhi ya mitaa ambayo watakuwa ni waelewa unaweza tumia muda wako kutafuta fundi aje kujenga lile daraja dogo lililovunjika au mkandasi kuzibua mtaro nk. Halafu wewe ukajipatika kiasi cha asilimia 10% ya kipato cha fundi uliyemtafuta kama shukrani yake kwako

Andika Makala fupi kujitangaza nia.


Kwa kuandika makala fupi inayomuelezea mtu mwenye uwezo wa kuwekeza kwako (donor) kufafanua ni aina gani ya biashara unajaribu kuanzisha na ina ya bidhaa na huduma utazokuwa unatoa na elezea jinsi biashara yako itavyowasaidia wateja unaowatazamia. Kupata mtaji wa biashara yako ni kitu kinachowezekana. Tuma makala hii kwa marafiki, familia, vyuoni na kwa wafanyabishara wadogo wenzako. Elezea vizuri faida za kukuunga mkono, faida ambazo zaweza kuwa kuwatangaza kwa wateja wako pale wanapohitaji huduma zinazendana na huduma wanazotoa wao, kupata kuwatanga katika Blog au tovuti yako au kupata fungu katika umiliki wa bishara yako (shares).  Hakikisha umekeka mawasiliano yako kama namba ya simu na barua pepe ili waweze kukutafuta endapo watakuwa na maswali ya kukuuliza kuhusu biashara yako au kutoa msaada wowote. Pia andika jinsi ya watu watavyoweza kukuchangia mfano akaunti ya benki, au huduma za simu kama MPESA etc.

     JIPATIE MAKALA KAMA HIZI KATIKA BARUA PEPE KILA WIKI

Enter your email address:


Delivered by BusinessTOK
Back To Top
Don't You Think this Awesome Post should be shared ??
| Best Ideas za kujitengenezea Mtaji wa kuanzisha Biashara ndogo Jijini Dar es Salaam. |