Makosa 7 yanayopelekea biashara nyingi kutofanikiwa.
Kuanzisha
biashara kwa watu wengi ni changamoto ambayo hawawezi kuikabili. Kuanzisha
biashara yako binafsi yaweza kukuletea faida kwa njia nyingi ikiwemo kujitambua
zaidi, kupata uhuru za kifedha (financial independence), fursa ya kuweka alama
(mark) katika maisha yako na pia kuwa katika nafasi ya kutoa mchango chanya
katika jamii yako au sehemu ya kibiashara.
Katika
kufikia hayo watu wengi hufikia kuanzisha biashara zenye mafanikio na nyingine
bila mafanikio. Makala hii inakuletea sababu tano za kwanini biashara nyingi
ndogo hushindwa kufanikiwa:-
1. Kutofanya
Utafiti wa kimasoko
Biashara
nyingi hushindwa kufanikiwa kwa sababu ya kutofanya utafiti wa kutosha wa
kimasoko (market) ambayo hupelekea mfanyabiashara kuingia katika biashara yenye
watu wafanyabiashara wengi tayari au biashara ambayo wateja hawapo na uelewa
mzuri juu yake, eneo (location) ambayo sio sahihi. Hasara ambazo mtu anaweza
pata kwa sababu ya kujiingiza katika biashara bila kufanya utafiti.
Bila
utafiti mfanyabiashara anaweza kuanza kuuza vifaa vya kisasa kama simu, Tablets
na computer katika kijiji kisicho na umeme au kuuza bidhaa maarufu kama adidas,
Gucci na Macintosh kwa wateja wasio na TV. Biashara yako inatakiwa iangalie
matatizo au watu wanachohitaji kutokana na mazingira yao.
2. Nafasi ya
kisheria ya biashara husika.
Kosa
lingine ni Mara nyingi wajasiriamali huingia katika biashara bila kufuatilia
sheria inasemaje juu ya biashara hiyo kwenye eneo analotaka kufanyia biashara,
wanashindwa kufuatilia taratibu za utunzaji wa mazingira na upatikanaji wa
ruhusa mfano biashara za kusafirisha mizigo, mkaa, na biashara ndogondogo
katika maeneo ya mijini (mfano, Dar es Salaam).
Pia
hapa tunazungumzia ulipaji wakodi au usajili wabiashara hiyo kupitia usajili wa
biashara ambayo sio sahihi kulinganisha na kipato cha biashara hiyo.
Mfanyabishara anatakiwa kufuatilia msamaha wa kodi na ajue ni usajili wa aina
ipi waweza kumsaidia kwa kumtoza kodi halali na yenye unafuu kutokana na umri
wa biashara yake na faida anayopata.
3. Eneo (location)
na kuwafikia wateja
Uamuzi
wa uuze wapi bidhaa zako ni rahisi, inatakiwa iwe eneo amablo watu wataweza
kukufikia kirahisi. Inatakiwa iwe located sehemu ambayo watu wana uhitaji wa
hiyo bidhaa. Iwe mahala ambapo wewe kama mfanyabiashara waweza pata bidhaa
unazouza au rasilimali za biashara yako kirahisi.
4. Kushindwa
kuanza kama biashara ndogo.
Ubora
wa bidhaa ni kuwa sahihi kwa lengo husika. Sio lazima kuanza biashara kwa
kununua flame au kununua duka ambalo ni Fixed Assets, watu wengi hujaribu
kuanza kwa kuwa mobile mara nyingine si kwa kupenda lakini hii husaidia
kutengeneza custumer base kabla hawajakuza biashara yake.
Biashara
ndogo ndogo zinazoanza bila Fixed Assets zinanafasi kubwa ya kukua na
kulitambua soko kuliko zile zinazoanza kwa fixed assets.
5. Kuwa na nidhamu
ya kifedha (Financial discipline)
Kuwa
mfanyabishara mkubwa unatakiwa kuwa na uelewa wa kujaza fomu na documents
nyingi mbalimbali za kimahesabu lakini haimaanishi kwamba utakuwa na uelewa wa
biashara yenyewe. Watu wanaweza kuanzisha biashara bila ya kuwa na uwezo
wakujaza au kusoma balance sheet au business plan.
Uelewa
kiasi wa vitu hivi ndio unaohitajika pale mfanyabiashara anapohitaji mkopo
huhitajika kwenda kueleza ni jinsi gani ataweza kutunza kiasi cha faida
atayopata kabla hajapata mkopo.
Wafanyabiashara
wadogo wadogo hukosa mikopo kwa kutojua jinsi ya kufanya mahesabu madogo na
kuwa na nidhamu katika uhifadhi wa pesa.
6. Kukosa Ushauri
wa mtu mwenye uzoefu (Mentor support, Second Opinion)
Wafanyabishara
wengi hukosa kujikosoa kwani kwa kuwa tupo katika nchi yenye watu masikini basi
wafanya biashara huweka eneo lake la biashara au bidhaa zake juu ya wateja na
kuwadhalau wateja. Mteja ni mfalme kwa hiyo mfanyabishara anatakiwa kujikosoa
kwa kuwauliza baadhi ya wateja wake kwa njia tofauti za kukusanya maoni.
Kwa
mtu kuamua kutumia pesa yake kwako yahitaji awe atambue unajali. Wafanyabishara
wengi wanashindwa kujua kwamba wateja wanatambua kuwa kitendo cha wao kununua
kwako wanachukua hatua ya kuwa-support na kudhani au kuwa-treat kana kwamba
wateja hao hawana sehemu nyingine ya kwenda kujipatia mahitaji hayo.
7. Teamwork and
Networking
Katika
ushindani ulipo sasa hivi ni vizuri mfanyabiashara kujiunga katika vikundi
mbalimbali ili aweze kujitangaza pamoja na kuwajua wafanyabishara wenzake ambao
wanaweza kumsaidia kwa mawazo na hata kwa wateja pale wanapoishiwa bidhaa Fulani
katika maduka yao.
Haya
ni makosa 7 ambayo wafanyabishara wadogo au wanaoanza huyafanya kwa kujua au
bila kujua. Kwa kufuatilia BusinessTOK utapata kuwasikiliza wafanya biashara
wataoweza kuongelea mada hii.
Usisite
kuweka maoni yako juu ya makala hii hapa chini.