
Kituo Kipya
Kwa nini vijana wa Kitanzania hawana uwezo wa kuziona fursa, wamezubaa sana, hawajui umuhimu wa kuwa wakwanza katika kufanya maamuzi. Leo hii wengi wa vijana wakianzania hawana utashi katika jambo lolote lile, wanazurula barabarani wakisubiri miujiza, leo ni siku ya tatu tangu nibandike tangazo hili la kuwasaidia na hakuna aliyenitafuta. Inamaana hata wazazi nao hawashughuliki kutafuta upenyo wa watoto wao, nao pia wanajidanganya kuwa muujiza wa mkopo utawatokea ama serikali italegeza masharti.
Mimi ninaanza darasa hata na watu wawili na sitafungua tena dirisha la kuandikisha. Wazazi wanakimbilia pre form one, kama walivyofanya miaka hiyo, hawana utashi wanatengeneza watoto wanofanana na wengine, hawajui dhana ya competition. Hata unapotoa offer ya kutmia muda wako wazazi wamebaki vipofu, wanataka vitu vya bure, ukiwaambia unawaita kuwaona wasanii, wazazi watawapa watoto na hela ya soda, huu ndio umasikini mnaoujenga kwenye familia zenu. Watanzania wengi watabaki na umasikini kwa kuwa wanaupenda na kuuzoea. Mpaka leo unangoja nini kumuandikisha mtoto wako kwenye kituo chetu? Tena wale wa tegeta wasio na uwezo wa hata nauli, wamelala wanangoja nafasi hizi zijazwe na wa mjini, mungu anisaidie nisiwe mmojawapo wa wazazi wapumbavu, maana watu hawa wameandikwa mpaka kwenye biblia, sawa na wale wanawali watano wapumbavu walioenda na taa zisizo na mafuta, mungu wasaidie wako