Bado vijana wa kitanzania hawajaamka kutafuta maisha,
Ni jambo la kushangaza sana kwamba vijana wa kitanzania wamekataa kuchukua hatua ya kubadilisha maisha yao. wanataka kazi lakini hawataki kabisa kujifunza nini cha kufanya ili kupata hizo kazi, Kazi ziko tele zinatangawa kila siku kwenye mitandao, waajiri wanatafuta watu wa kuwaajiria vijana wamekaa nyumbani hawataki kujifunza. Nashukuru sana kwa wale wachache waliohudhuria kozi yetu pale Regency Park Hotel, mikocheni, ninaamini walijifunza kitu na wengine tunaendelea kuwasaidia katika ktuengeneza proposal zao za biashara, wengine wamehudhuria zile interview walizokuwa wanatarajia kwa kufanikiwa, wengine wameanza kuitwa kwenye usaili kwa kuwa hata barua zao za usaili wamebadilsha namna yakuziandikisha. Lakini wengine mamia bado mko huko vijiweni mnapiga domo na siku zinaekwenda. Tukufanyie nini? Hakuna chochote under the sun utakachoweza kufanya kama huna skills zinazotakiwa, vijana wengi mmejaa uvivu na mnategemea miujiza, hata hiyo miujiza haiwezi kuwafuata vyumbani mliko. Tunaendelea na vipindi vya mafunzo chuoni kwetu maalumu kwa vijana waliomaliza form four na pengine hawakufanikiwa kupata grade za kuwapeleka form five, tunajua mko wengi sana na bado mmekaa majumbani, ninatamani hata wazazi wenu wangehusika na maisha yenu maana wakati wa kutengeneza ni huu, muda ukipita hutakua na nafasi tena, tuna nafasi 10 tunataka kuchukua vijana wa kuwafundisha project management kwa ktumia computer, masomo ni ya mwezi mmoja tu wa April, na malipo ni sh 100,000/- kwa huo mwezi. hakuna namna ya sisi kuwapatia masomo bure, kuna garama za uendeshaji, kama uko tayari kupata kitu tofauti mwezi huu tupigie simu na ufike kujiandikisha. idadi ya wanafunzi tunayochukua ni sawa na idadi ya computer tulizo nazo.Natumaini dalili ziko wazi huko tunakokwenda hakuna tena ubabaishaji wa mtu kupata kazi yoyote kwa mjomba ama shangazi ama kwa jina la baba, serikali ya awamu ya tano iko serious na elimu, njoo walau upate pa kuanzia, tupo kwa ajil yako kama hutatutumia hasara ni yako