MAFUNZO YATAKAYOBADILISHA MAISHA YAKO - JIANDIKISHE LEO
FAHAMU KUHUSU EABMTI
KUHUSU (EABMTI) ni
kampuni ya biashara ya Kiimataifa inayofanya kazi za Habari na Mahusiano ya
Umma, Biashara Mafunzo kwa makampuni Binafsi, Mashirika ya Umma, Vikundi na Mtu
mmoja mmoja nchini. Tangu ilipoanzishwa mwezi January mwaka 2009, kampuni yetu
imeshafanya kazi na makampuni zaidi ya 100 ya hapa nchini Tanzania, nchi za
Afrika Mashariki na hata Nje ya bara la Afrika
DIRA YETU ni
kuwezesha kutoa mafunzo ili kuwafanya vijana wa kitanzania na wengine, kuanza
kufikiri kama wafanyabiashara waliofanikiwa, ili kuwawezesha kufanyanya maamuzi
sahihi na kwa wakati sahahi, katika kila eneo la maisha yao. Kuwatambua vijana
wa Kitanzania, Wa kike na Wakiume, wenye shauku ya ujasiriamali, kutambua vyao
na kuvigeuza kuwa mchanganua wa biashara ulio tayari kuwekwa sokoni.
TUNATOA MAFUNZO KWA VIJANA
kituo chetu kinatoa mafunzo ya vitendo kwa vijana. Kwa bahati mbaya sana Elimu ya Tanzania imeshindwa kuvutia soko la ajira kwa kuwa wahitimu wake wanaonekana kutokuelewa kabisa mahitaji ya soko. Ndio maana vijana wa vyuo vikuu wanashindwa kupata ajira ijapokuwa uchumi wa Tanzania unakua kila siku, na uwekezaji unazalisha kazi nyingi na nzuri kila siku. Tunatambua kuwa zaidi ya asilimia 75 ya ajira za juu (CEOs) zimeshikwa na wageni. Ajira za kawaida pia zinapokwa na wageni wenye elimu ya chini kuliko wahitimu wetu wa vyuo vikuu. Pamoja na msururu wa vyuo na vyo vikuu Tanzania, bado havijaweza kujibu mahitaji ya soko. NI kwa sababu hii sisi EABMTI, chini ya uongozi wa mkuu wetu bi Rosemary Mwakitwange, tumeamua kutengeneza curriculum itakayo zalisha vijana walioandaliwa kujibu mahitaji ya soko la sasa. Ni mafunzo ya muda mfupi yatakayokuweka vizuri sokoni, pia tutakuonyesha aina ya maswali wanayouliza waajira, hakuna chuo kinachojua siri hii kwa kuwa wakufunzi wetu wengi wao, hawajawahi kuajiriwa katika soko hili na hawataweza kujua mahitaji ya waajiri. Sisi tumepita huko, na hata sasa tunashirikishwa katika mchakato wa ajira kama wataalamu (consultants). Tunataka kutengeneza vijana waliofundishwa mbinu za kupambana katika soko la ajira na kushinda. Tumeandaa kozi za aina mbili kwa makundi ya vijana yafuatayo:
1) WAHITIMU WA KIDATO CHA 4 NA CHA 6 WANAOTEGEMEA KUENDELEA NA MASOMO
LENGO KUU: Lengo kuu la mafunzo haya ni kuwaandaa vijana wanaotegemea kuendelea na masomo ya high school, vyuoni, ama Vyuo Vikuu. Mafunzo haya yatawasaidia washiriki kuelewa kwa undani habari ya masomo wanayokwenda kuendelea nayo ili kuthibitisha kuwa yanawapeleka kwenye hatima waliyopanga. Hii inamaana je, kwa masomo hayo ni kweli yatawawezesha kufanya kazi wanazozipenda? ili kama sio basi waweze mapema ama kubadilisha masomo au kubadilisha malengo ya kazi wanazozitaka. Itawapa utulivu na amani katika katika kuendelea kwao.
FAHAMU kuwa kuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya masomo yako ya high school, na ile kazi unayoitaka maishani. Kufahamu jambo hili mapema kutakuongezea nguvu ya kujiandaa katika miaka hiyo miwili utakayokuwa katika masomo ya high school na hivyo kutafuta hata mbiinu mbadala wakati huo wa kujiongezea ufahamu katika masomo yako badala ya kutegemea mafunzo ya mwalimu wa masomo peke yake.
Mafunzo yatakayotolewa ni pamoja na:
- Mbinu za Mawasiliano ikiwemo kuandaa taarifa za masomo na kuziwakilisha mbele ya jamii (Presentation skills and Public Speaking)
- Matumizi ya Computer katika kuandaa na kuwasilisha taarifa za masomo. Washiriki watafundishwa programs za Power Point na movie maker ili kuzitumia katika kuwasilisha taarifa za shule
- Siri ya Mwanafunzi aliyefanikiwa - Washiriki watasaidiwa kujenga uwezo katika kujiamini (Confidence) , Kuwa na uwezo wa hali ya juu katika eneo lao la masomo (competence) na kuwa na mtazamo usioyumba ( consistence).
- Wahitimu watapatiwa vyeti vya Ushiriki
Angalizo:
Mara nyingi tunaona kuwa vijana wanapomaliza high school, hawana ufahamu wakutosha juu ya nini wakasome ili kufikia hatima yao kikazi. Na kwa mtindo huu wa masomo kupangwa na bodi, tumeona vijana wengi wakipangiwa specializations ambazo hata kujua zitakapo wapeleka. Na wakati mwingine, kutojua mambo mengi yaliyomo kwenye shahada Fulani na hivyo kuishia kuona udogo waka na kuidharau. Mfano mzuri ni wa wale wanafunzi wa Mass Com ambao wao wanafikiri kubobea huko hakuna nafasi nyingine zaidi ya kuwa mwandishi wa habari. Mafunzo haya hivyo basi, yatatoa nafasi ya mwanafunzi kupembua na kuwa na taarifa kamili juu ya kila ‘ specialisation’ na hivyo kwa
wakati mufaka kutambua kama je anachokisomea kitamfikisha kwenye kazi anayoitaka?
2) WAHITIMU WASIOENDELEA NA ELIMU YA JUU
Mradi huu ni maalumu kwa vijana wasio na ujuzi wowote, na pengine hawana muelekeo wowote wa ajira lakini wanataka kupata mahali pa Kuanzia. Hawa vijana wako wengi, na wanahusisha pia vijana ambao wanataka kufanya biashara. Haijalishi una ujuzi wowote ama huna, huu mradi umekulenga wewe ili kukupatia mahali pa kuanzia. Yawezekana unataka kufanya biashara lakini hujui mahali pa kuanzia, huu mradi ni kwa ajili yako. Yawezekana umejaribu kufanya biashara mara kadhaa bila mafanikio, wewe pia unatuhusu. Yawezekana unalo wazo la biashara lakini hujui uanzie wapi, karibu sana wewe ni mlengwa wetu. yawezekana pia hujui hata la kufanya, tunakukaribisha sana.
Kozi hii ya miezi mitatu (3) ni ya hatua ya kwanza, mhitimu anaweza kuchagua kozi nyingine atakazozipenda baada ya kuhitimu hatua hii. Mafunzo yatakayotolewa katika hatua hii ya kwanza ni panoja na:
- Kujitambua na kufahamu shughuli unayotaka kuifanya. Yaweza kuwa ni biashara, au kilimo au kazi, au ktafuta nafasi za kusoma zaidi
- Kuandaa wazo la biashara
- Kugeuza wazo lako la biashara kuwa mpango wa biashara (Business Plan)
- kutoka na picha kamili ya nini unachotaka kufanya katika maisha yako
- Mafunzo ya computer kwa wanaoanza
- Kila mhitimu atapatiwa cheti cha Ushiriki
Malipo kwa masomo haya ni shilingi laki moja kwa kila mwezi kwa jumla ya miezi 3.
Jinsi ya
kujiandikisha, tuandikie kwa barua pepe
kwenda kwa info@eabmti.co.tz , au piga
simu ya mezani nambari +255-222-602-608, Tembelea tovuti yetu kupitia
www.eabmti.co.tz , facebook , na blog yetu at BizzTOKK
MASOMO
YATAKAYOFUNDISHWA:
- Kujitambua ili kufahamu utashi wao juu ya ujasiriamali na kazi za biashara.
- Kuandaa wazo la Basher
- Jinsi ya kuwa Mfanyabiashara mwenye Mafanikio - Mbinu za kufanya biashara kwa mafanikio
- Mbinu za Mawasiliano na Lugha ya Biashara
- Kuandaa Mpango wa Biashara - Business Plan
- Mafunzo ya Computer kwa Mfanyabiashara Mdogo
Cheti cha Mafunzo;
Mhitimu atapatiwa cheti cha ushiriki kutoka kwenye Chuo
Chetu, cheti kitkachodhibitisha kuwa Mwanafunzo huyo ameshiriki mafunzo ya
Ujasiriamali katika mbinu mbali mbali na kufaulu